Total Pageviews

Sunday, April 17, 2016

AMISOM yaomba msamaha kwa kuwauwa kwa bahati mbaya raia

Ujumbe wa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kwa Somalia AMISOM, umeomba msamaha baada ya kuwauwa kwa bahati mbaya raia wanne waliowadhania kuwa ni wapiganaji wa kundi la kigaidi la al-Shabab. Tukio hilo limetokea katika eneo la Buulo Mareer kilomita 80 kusini mwa mji wa Mogadishu.

 

Ujumbe wa AMISOM umefunguliwa uchunguzi wa kubaini hali halisi ya mauwaji hayo, baada ya tukio hilo kuripotiwa kwa tume ya Umoja wa Afrika. Zaidi ya wanajeshi 22,000 wametumwa nchini Somalia, kuisaidia serikali ya nchi hiyo kuimarisha usalama na kupambana na mashambulizi ya kundi la kigaidi la al-Shabab.

Mwaka 2011 wanajeshi wa AMISOM walifanikiwa kuwatimuwa wapiganaji wa al-Shabab, kutoka mji mkuu wa Mogadishu. Hata hivyo katika miezi ya karibuni kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara mjini humo, likinufaika na kupungua nguvu kwa ujumbe huwo pamoja na udhaifu uliyomo ndani ya serikali ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment