Total Pageviews

Sunday, April 17, 2016

Wawakilishi wa OPEC kusaini mpango wa kupunguza uzalishaji wa mafuta

Wawakilishi wa mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani wamekutana leo hii nchini Qatar, kutafuta muafaka wa uwezekano wa kupunguza uzalishaji unaotarajiwa kusaidia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo iliyoporomok

Hata hivyo uhasama wa muda mrefu baina ya Saudi Arabia na Iran umeugubika mkutano huwo. Iran haikutuma mwakilishi wake, kutokana na kwamba haitoshiriki katika mpango wa kupunguza uzalishaji wa mafuta kwavile kwa muda mrefu ilifungiwa soko hilo kufuatia vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na nchi za magharibi.

 Hata hivyo Saudi Arabia imesema itagoma kusaini mpango huwo hadi pale Iran itakaposhiriki. Mkutano huwo umehudhuriwa na wawakilishi wa nchi 15. Wengi wanachama wa Shirika linalosafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC, linaloongozwa na Saudia Arabia. Halikadhalika nchi nyengine zisizo wanachama kama vile Urusi zmeshiriki mkutano huwo.

No comments:

Post a Comment