Viwambo
kutoka kamera za CCTV za uwanja wa ndege wa Brussels, zikionyesha "mtu
mwenye kofia," Mohamed Abrini, mtuhumiwa wa tatu wa mashambulizi ya
mjini Brussels.
Assia anasema, wakati alikubali kumpokea na kumpa hifadhi mtu
aliekutana naye katika mgahawa, Aprili 5, hakujua kabisa kuwa ni
Mohamed Abrini, mtuhumiwa wa mashambulizi ya mjini Paris na Brussels, na
alikua akitafutwa na polisi zote za Ulaya.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 43, aliachiliwa huru siku
mbili baada ya kuzuiliwa nyumbani kwake. Alizuiliwa nyumbani kwake baada
ya Mohamed Abrini kukamatwa. Assia aliposikilizwa na majaji, alisema
hakuweza kumtambua Mohamed Abrini
"Kijana tu kama hivi, siningeweza kuwa na mashaka naye kwamba ni mtu anayetafutwa," Assia ameiambia runinga ya BFM TV. "Alikuwa mtu wa kawaida. Labda alikua ameficha tabia yake. Katika siku mbili, huwezi kumjua mtu."
Mohamed Abrini alikua na Fedha nyingi
Mohamed Abrini alibaki usiku mmoja na nyumbani kwake, Assia amesema. Kwa mujibu wa Assia, Abrini aliweza kumwambia kuwa alisahau kadi yake ya uraia kwa wazazi wake, ambao walikuwa nchini Ujerumani. Maelezo mengine muhimu, kijana huyo alionekana kuwa na fedha nyingi. "Alikuwa na fedha, fedha nyingi hasa, Assia anakumbuka. Alikuwa na pesa nyingi za 50 na za 20."

No comments:
Post a Comment