Total Pageviews

Friday, April 8, 2016

Raia wawili wa china kotini kwa kukwepa kulipa kodi

Dar es salaam, Raia wawili wa china Mjun na Huifang ma, wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ilala war es saakikabiliwa na mashitaka mawili likiwamo la kushindwa kutumia mashine za kutolea risiti za kielectronic maaraufu kama EFDs katika biashara zao.

wachina hao ambao wote ni wafanyabiashara na wakazi wa mtaa wa narung'ombe kariakoo pia wanakabiliwa na shitaka la kushindwa kuzisajili biashara zao katika kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT.
mshitakiwa wa kwanza (Ma jun) katika kesi hiyo hakuwepo mahakamani kwa madai ya kuwa yuko nje ya nchi na upande wa jamhuri umeiomba mahakama hati (arrest warrant) ya kumkamata mshitakiwa huyo

   


Mfanyabiashara Raia wa Kichina, Huifang Ma
                Mshtakiwa namba 2 Huifang Ma akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi

Wakili kutoka mamlaka ya mapato Tanzania alidai mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Saidi mkasiwa kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo machi 23 mwaka huu
Washitakiwa hao ambao ni wamiliki wa kampuni ya HM TEXTILE CO. LTD iliyoko block 54 kiwanja namba 6 kilichopo mtaa wa aggrey eneo la kariakoo

Hata hivyo mshitakiwa namba 2 Huifang alikiri shtaka la kwanza na kukataa la pili.. Mshitakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana ya shilingi milioni 3 na kupelekwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena april 21 mwaka huu

No comments:

Post a Comment