Rais wa Ufaransa, François Hollandeakimpokea Ikulu ya Elyséemwenzake wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Jumatau Aprili 4, 2016.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekosoa kauli ya kinara wa
muungano wa upinzani na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, kuwa hatua
ya Mahakama ya Kimataifa ya ICC kutupilia mbali kesi dhidi yake Kenyatta
na naibu wake William Ruto si sahihi.
Akizungumza akiwa nchini Ufaransa, Odinga alisema hatua hiyo ya
ICC ilkuwa ni pigo kwa jitihada za kupigania haki hasa baada ya
uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007.
Rais Kenyatta anasema, matamshi ya Odinga yanalenga kuwaharibia jina.
Kauli ya Kenyatta imeungwa mkono na Naibu wake Ruto ambaye amesema wale waliomsingizia wameshindwa.
Aden Duale naye ni kiongozi wa walio wengi bungeni, amepomgeza msimamo wa viongozi hao wawili.
Mahakama ya ICC ilisitisha kesi dhidi ya viongozi wa Kenya kwa ukosefu wa ushahidi.

No comments:
Post a Comment