Azam
FC imejiweka kwenye nafasi ya kuvuka mchujo wa kuwania kupangwa kwenye
makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika barani Afrika, baada ya ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Esperance ya Tunisia jioni ya leo katika mchezo wa
kwanza wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Jijini Dar es Salaam.
Shukrani kwao, wachezaji vijana wadogo Farid Mussa Malik na Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ waliofunga mabao hayo kipindi cha pili baada ya Azam FC kuwa nyuma kwa bao 1-0 tangu kipindi cha kwanza.
Esperanace walipata bao lao dakika ya 33 kupitia kwa Haithem Jouini aliyefunga kwa kichwa akimalizia krosi ya Ilheb Mbaark.Kipindi cha pili, Azam FC walifanikiwa kubadilisha matokeo ya mchezo kutoka kuwa nyuma kwa bao 1-0 hadi kuongoza kwa mabao 2-1.
Farid alianza kufunga dakika ya 68 baada ya kutanguliziwa pasi fupi na Singano Messi. Messi akaifungia bao la ushindi Azam dakika ya 70, safari hiyo naye akitengenezewa na Farid Mussa kwa krosi nzuri kutoka upande wa kushoto.
Azam FC, sasa inatakiwa kwenda kulazimisha sare yoyote ugenini katika mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kwenda hatua ya mwisho ya kuwania kucheza hatua ya makundi.

No comments:
Post a Comment