Wapiganaji wa kundi la waasi wa FDLR washambulia kituo cha polisi nchini Rwanda.

Wapiganaji wa kundi la waasi wa FDLR washambulia kituo cha polisi nchini Rwanda.
Kulingana na naibu msemaji wa jeshi la Rwanda Luteni kanali Rene Ngendahimana,wapiganaji wanaokadiriwa kuwa kati ya 20 na 30 wa FDLR wamevuka eneo hilo la mpakani mnamo usiku wa manane kuamkia leo na kushambulia kituo hicho cha polisi.

Mwezi uliopita,eneo hilo pia lilishambuliwa na wapiganaji waliotajwa kuwa wa kundi la FDLR ambapo taarifa ya jeshi la Rwanda ilisema kuwa mpiganaji mmoja wa FDLR aliuawa.
No comments:
Post a Comment