Jumla ya wanafunzi 62 wa chuo kikuu
cha Nairobi nchini Kenya wamefukuzwa kutoka chuo hicho, baada ya
kushuhudiwa ghasia zilizosababisa kufungwa kwa chuo kwa muda usio
julikana wiki moja iliyopita.
Wanafunzi waliteketeza kwa moto
afisi za chuo hicho kutokana na kile kinachotajwa kuwa matokeo ya
uchaguzi wa kumchagua kiongozi wa wanafunzi chuoni.Chuo kikuu cha Nairobi kiliseme kuwa kilichukua hatua hizo za kinidhamu dhidi ya wanafunzi walioshiriki katika kuharibu mali ya umma.

Chuo cha Nairobi kilikumbwa na ghasia zilizotokana na uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment