Habari yoyote ile kwetu ni habari muhimu kwa lugha yoyote ile na mahala popote pale
Total Pageviews
Sunday, April 17, 2016
Annan: Nkurunziza hakustahili kuwania urais
Aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa
mataifa bwana Kofi Annan amemkosoa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa
kuwania muhula wa tatu.
Bw Annan amesema Nkurunziza anafahamu
vyema kuwa ni kinyume cha katiba ya taifa hilo kuwania madaraka kwa
zaidi ya vipindi viwili.
Raia huyo wa Ghana anamlaumu rais Nkurunziza kwa
kusababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu mia nne
Raia huyo wa Ghana anamlaumu rais Nkurunziza kwa kusababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu mia nne.
Bw
Annan ameiambia BBC kuwa bw Nkurunziza haoneshi dalili zozote za
kutafuta suluhu la amani wala nia ya kutaka mazungumzo ya kweli na
wapinzani wake. Bw Annan ameiambia BBC kuwa bw Nkurunziza haoneshi dalili zozote za kutafuta suluhu la amani
Katibu huyo wa zamani ameiomba jamii ya imataifa
kuyasaidia mataifa ya Afrika yanayokabiliwa na matatizo chungu nzima
kama vile Ethiopia inayokabiliwa na baa la njaa
Annan anasema
kuwa mataifa hayo ya Afrika yamesahaulika huku kurunzi ya ulimwengu
ikiangazia Syria na mataifa ya Mashariki ya kati.
No comments:
Post a Comment