Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi kanda maalumu Simon Sirro amesema, miongoni mwa majambazi waliokamatwa ni Ibrahim Juma(31) mkazi wa Kiwalani Kigilagila, Samweli Mbonea (40) Fundi gereji Mkazi wa Kiwalani pamoja na Anthony Kanywenywe (60) Mwindaji na mkazi wa Kiwalani.
Amesema majambazi hao walikutwa na taa kubwa nne za magari, pawa windo moja na nati za magari na watuhumiwa sita kati ya waliokamatwa wamekiri kushiriki katika matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali likiwemo la Riki Hill Hotel katikati ya jiji na Lake oil Buguruni.
No comments:
Post a Comment