Marekani imelaani, kile ilichoeleza
kuwa hatua kali zilizochukuliwa na serikali ya Gambia, kupambana na
maandamano ya amani yaliyofanyika huko.
Waziri wa habari wa Gambia, Sheriff Bojang , alisema wale waliokamatwa, waliandamana kinyume cha sheria.

Kati yao alikuwa kiongozi wa upinzani, Ousainou Darboe.
Taarifa ya Marekani, haikutaja kifo cha mwanasiasa mwengine wa upinzani, Solo Sandeng, kinachosemekana kutokea gerezani ambacho kilizusha maandamano ya jana.
Waziri huyo wa Gambia, aliiambia BBC, kwamba hawezi kuthibitisha kama Bwana Sandeng amefariki au la.
No comments:
Post a Comment