Total Pageviews

Sunday, April 17, 2016

Brazil: Chuma cha rais Rousseff ki motoni

 

Maandamano makubwa yanapangwa kufanywa sehemu mbalimbali Brazil, ambako wabunge wanatarajiwa kupiga kura leo, ikiwa wanataka Rais Dilma Rousseff ashtakiwe au la, kwa sababu ya kubadilisha bajeti. Wanaompinga lazima wapate thuluthi mbili ya kura zote , kuweza kumshtaki rasmi kiongozi huyo katika baraza la Seneti.
Wanaompinga lazima wapate thuluthi mbili ya kura zote , kuweza kumshtaki rasmi kiongozi huyo katika baraza la Seneti.
Mamia ya askari polisi wenye silaha wameshika zamu, kujaribu kuzuwia makabiliano baina ya waandamanaji wanaopingana, na ambao wamekesha nje katika mji mkuu, Brasilia.
Waandishi wa habari wanasema, kizuizi cha urefu wa mita mbili, kilichowekwa baina ya waandamanaji hao, mahasimu ni ishara ya mgawanyiko mkubwa nchini, baina ya wafuasi na wapinzani wa Rais Rousseff.
                    Bi Rouissef anakanusha kuwa alibadilisha hesabu za bajeti
Bi Rouissef anakanusha kuwa alibadilisha hesabu za bajeti, kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014, ambapo alichaguliwa tena.
Anawashutumu wanasiasa wanaotaka kuitoa madarakani serikali iliyochaguliwa.

No comments:

Post a Comment